15/04/2024
Triumph (2021)
iMDb: 5.8
Genre: Drama
Runtime: 1h 40mins
Rating: PG13
Starring: RJ Mite, Terrence Howard, Jonathon Schaech, Colton Haynes, na wengine
Storyline: hizi ndio zile filamu ambazo unapenda kuangalia na familia ikajifunza kitu kizuri namna ya kuishi na watu wa makundi maalum katika jamii yetu hiiihii kwani na wao ni watu k**a sisi na wanastaili kupewa nafasi katika kila nyanja ikiwemo michezo.
Hapa utafurahia mchezo wa masumbwi miaka hio ya 80 ulivyokuwa muhimu katika kuleta matumaini ya ndoto za mafanikio kwa kijana Mike, ambaye alizaliwa akiwa na mtindio wa ubongo kwa kukosa oksijeni ya kutosha pindi tuu alipozaliwa..
Utakachokifurahia zaidi katika filamu hii ni vile Terrence Howard alivyozinasua zile speeches zake za kimarekani na kuendana vilivyo na maudhui ya humu ndani.
Nimependa pia kumuona, Colton Hayes, huyu alitamba kwenye Arrow k**a sidekick wa Green arrow, jamaa anajua alafu anajua tena...maana ameigiza vizuri sana k**a kaka mwema na rafiki mzuri sana, licha ya utanashati alionao
Maadili humu ndani ni ya kiwango cha juu mno, maana kuanzia lugha, mavazi, na maudhui kwa ujumla ni ya kiwango cha juu,
Ninashauri inapaswa kuangaliea na rika la watu wote na inahamasisha jamii youote ile funiani kuishi vyema na kila mtu, pasipo kumchukulia udhaifu wake wa kimwili au akili.
NB: steringi haumwi wala hana tatizo lolote lile la afya ya akili, usidanganyike, jamaa anajua sana kuigiza yaaniππππ
Enjoy.