21/08/2026
Jana ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa. Namshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha na kwa kuniongezea mwaka mwingine.
Nilipokea ujumbe mmoja tu kutoka kwa dada yangu, na mwingine nikaupata leo kwa kuchelewa kutoka kwa dada yangu mwingine.
Niliwashukuru kwa moyo wangu wote, kwa sababu ujumbe mmoja kutoka kwa mtu anayekukumbuka una thamani kubwa.
Lakini ukweli ni kwamba, jana ilinifanya nitafakari pia kuhusu wale niliofikiria wangekumbuka lakini hawakufanya hivyo.
Sina hasira na mtu, wala sitaki kumlaumu yeyote, Kila mmoja ana maisha yake, changamoto zake na mambo ambayo huenda mimi siyajui.
Badala ya kulalamika, nimechagua kulichukua hili k**a somo,
Wakati mwingine kinachotuuma si kile ambacho watu wamefanya, bali ni kile ambacho mioyo yetu ilitarajia kutoka kwao.
Nimejifunza kwamba si kila mtu tunayemweka moyoni mwetu ametuweka mahali pale pale. Na hilo ni jambo ambalo tunapaswa kulikubali kwa amani, bila chuki.
Kwa dada zangu mlionikumbuka, asanteni sana,
na kwa wale ambao hamkunikumbuka, nanyi asanteni.
Labda bila kujua, mmenifundisha kupunguza matarajio yangu kwa wanadamu na kuongeza shukrani yangu kwa Mungu.
Thamani yangu haipungui kwa sababu simu haikupigwa,wala kwa sababu ujumbe haukuja.
Bado nina maisha, ndoto, kazi, watu ninaowapenda na sababu nyingi za kumshukuru Mungu.
Kwa hiyo sitaikumbuka jana k**a siku ambayo watu walinisahau, bali k**a siku ambayo maisha yalinifundisha jambo muhimu kuhusu watu, matarajio na moyo wangu.
Mwaka huu mpya wa maisha yangu nauanza kwa shukrani, amani na moyo mwepesi.
Happy Birthday to me. β€οΈ
Mwaka mpya wa maisha.
Moyo ule ule, lakini katika funzo zaidi.ππ